Sikh Union Nairobi Yazidi Kukomaa Magongo ya Masters Series
- heartmediak4
- Sep 3, 2024
- 2 min read
Na HEART MEDIA
Jumanne, 3 Septemba 2024

WACHEZAJI wa timu ya magongo ya Masters Series ya Sikh Union Nairobi wameonyesha wanazidi kuimarisha mchezo wao baada ya kutawazwa mabingwa wa taji la michuano ya makala ya mwaka huu. Timu hiyo ndio ya kwanza kubeba taji hilo kwa mara ya pili tangia mchezo huo huanzishwe nchini mwaka 2019. Tangia kipindi hicho taji hilo limebeba na tofauti. Sikh Union Nairobi iliadhibu Nakuru Masters kwa mabao 2-1 kupitia mipigo ya matuta baada ya kutoka sare tasa katika fainali ugani Dashmesh Stadium, Nairobi. ''Tuna furaha tele kushinda taji hilo kwa mara ya pili maana mwanzo tulibeba mwaka uliyopita,'' alisema kocha wa Sikh Union Nairobi, Inderjit Singh Matharu. Aliongeza kuwa kufuatia ufanisi huo wamepania kujituma kisabuni kupigania kutetea kombe hilo kwenye makala yajayo. Hata hivyo alidokeza kuwa imekua vigumu sana kushinda taji hilo mfululizo kwa kuzingatia washiriki wamekuwa wakishusha upinzani mkali.
Timu zote nne zilizoshiriki nusu fainali ya shindano hilo ziliwahi kuibuka mabingwa wa michuano ya kinyang'anyiro hicho. Kwenye nusu fainali Sikh Union Nairobi ilirarua Goan Institute kwa mabao 3-1. Wafungaji wa Sikh Union Nairobi walikuwa Wilson Otieno, Arif Shan na Jackie Mwangi. Naye Joshua Njogu alifungia Goan Institute bao la kufuatia machozi. Kwenye nusu fainali ya pili, Harvinder Singh alitikisa wavu mara moja na kubeba Nakuru Masters kuangusha Parkroad Lions kwa bao 1-0. Katika msimamo wa mechi za mchujo Kundi A, Goan institute iliibuka kidede mbele ya Parkroad Lions. Nayo Nakuru Masters iliibuka ya kwanza na kufuatia na Sikh Union Nairobi Kundi B.
Shindano hilo limevutia timu kumi zikiwa: Nakuru Masters, Green Sharks, Wazalendo Veterans, Impala Veterans, Kisumu Veterans, Sikh Union Club Nairobi na Goan Institute. Zingine ni Parkroad Lions, Western Masters na Blue Ocean Chiefs.


