Shofco Pabaya Kwenye Mbio za Ruben FM Huku Creative Hands, Kamongo Zikitamba
- heartmediak4
- Aug 27, 2024
- 1 min read
Na HEART MEDIA
Jumanne, 27 Agosti 2024
SHOFCO Mukuru FC imejipata hoi kwenye kampeni za kuwania taji la Ruben FM Cup baada ya kutoka bao 1-1 na Vision FC kwenye mechi zilizochezwa Jumapili tarehe 25 Agosti ugani Vision Embakasi, Nairobi. Nazo Kamongo FC na Creative Hands kila moja ilitwaa pointi tatu na kukaa pazuri kusonga mbele. Kamongo iliadhibu Rising City kwa mabao 2-1 huku Creative Hands ikisajili ushindi sawa na huo mbele ya City Foxes. Shofco Mukuru imeondoka kampeni hizo kwa kuzingatia kwenye mechi ya uatngulizi ilicharazwa mabao 3-1 na Mukuru Wazee FC.

Kamongo FC ya kocha, Enock Mukoma ilipata ufanisi huo kupitia Edwin Maina aliyetikisa wavu mara mbili. Naye Stephen Osengo alifungia Rising City bao la kufutia machozi. ''Vijana wangu walishusha soka la kuvutia na kufanikiwa kusajili alama tatu muhimu,'' anasema kocha wa Kamongo FC. Licha ya hayo anaongeza kuwa watahitaji kuzima wapinzani wao kwenye mechi ya mwisho katika kundi lao. Kamongo FC ilitoka nuguvu sawa bao 1-1 na Creative Hands kwenye mechi ya utangulizi.

Nayo Creative Hands ilionyesha wazi kuwa inataka kubeba taji hilo ilipopata ushindi huo kupitia Samuel Kigo na Caleb Abuga. Naye Leonard Pariot alifungia City Foxes inayokaribia kuondokea ngarambe hiyo.
Kwenye matokeo hayo, Brian Mwania alicheka na wavu mara moja na kubeba Wilsom Aviators kudunga Young Warriors kwa bao 1-0. AFC Leopards Embakasi Branch iliona giza iliponyukwa mabao 2-1 na Ruben United. Wafungaji wa Ruben United walikuwa Fredrick Onyango na Christopher Milo. Naye Franklin Mutei alifungia AFC Leopards bao la pekee


