top of page
Search

Ruben FM Cup: Meteorite, Real Warriors, United Kings Zatamba

  • heartmediak4
  • Aug 25, 2024
  • 2 min read

Na HEART MEDIA

Jumapili, 25 Agosti 2024.





MICHUANO ya makala ya saba kuwania taji la Ruben FM Cup inaendelea kuchacha huku washiriki wakizidi kupambana kiume kufukuzia tiketi za kufuzu kwa hatua ya 16 bora. Kwenye mechi zilizochezwa Jumamosi tarehe 24 Agosti, United Kings ilibeba ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Busec ugani Ruben, Embakasi Nairobi. Vijana wa United Kings walionyesha mechi safi na kubeba ufanisi huo kupitia juhudi zake Ismail Abdi aliyepiga 'hat trick, nao Samuel Kimani na Daniel John kila mmoja alifunga mabao mawili. Upande wa Busec Chris Nyandemo na felix Ndolo kila mmoja alicheka na wavu mara moja.


Kwenye uwanja wa Vision, Meteorie FC ilipiga Dream Team mabao 2-1 ikiwa ni ushindi wa pili na kujiweka pazuri kusonga mbele endapo itashinda ama kutoka nguvu sawa kwenye mechi ya tatu. Meteorite ilijitahidi kwa udi na uvumba licha ya kucheza na wapinzani wao ambao hawafahamu mchezo wao na kufanikiwa kuzoa alama tatu muhimu. Mabao ya meteorite yalitupiwa kimiani na Philip Omasaja na Sylvester Patrick. Nayo Dream Team ilipata bao la kufutia machozi kupitia Joash Ochida. ''Ninapongeza wachezaji wangu kwa kazi nzuri waliofanya kwenye mchezo huo uliokuwa mgumu zaidi kwetu,'' anasema meneja wa Meteorite, Harman Thungu. Anaongeza kuwa wanazidi kusoma wapinzani kwa mechi kwa kuzingatia ndio mwanzo wanaoshirii ngarambe hiyo. Kwenye utangulizi wa mechi zao walidunga Ruben United kwa bao 1-0.


Kwenye mfululizo wa kipute hicho, Eric Omulepu alitikisa wavu mara moja na kubeba Gateway FC kuangusha Milan FC kwa bao 1-0 ugani Embakasi Girls.

Nayo Real Warriors ilipepeta Simba FC kwa magoli 2-1. Javan Mokoya wa Real Warriors alifunga mabao hayo mawili huku Sebastian Masheti akifungia Simba bao la kufuatia machozi. Mshindi wa makala ya mwaka huu kitengo cha wanaume atatuzwa Sh100,000 huku bingwa wa kina dada akitia kibindoni Sh40,000.

 
 
bottom of page