Ngarambe ya Koth Biro Yazinduliwa
- heartmediak4
- Aug 20, 2024
- 1 min read
Na HEART MEDIA
Jumanne, 20 Agosti 2024

MABINGWA wa michuano ya Kothbiro, Pumwani Sports United wamelazimishwa kutoka nguvu sawa bao 1-1 na Ziwani All Stars kwenye nechi ya kuzindua ngarambe ya makala ya 47 ugani Umeme, Ziwani Nairobi. Pumwani Sports ilitwaa taji la makala yaliyopita kwa kuzaba Kingstone FC mabao 2-0 katika fainali ya kusisimua iliyoandaliwa ugani humo. ''Kampeni za muhula huu zimepangwa kukunjua jamvi wikendi ijayo,''anasema ofisa wa kamati andalizi, Issa Barugote. Anaongeza kuwa droo ya timu zinazotarajia kushiriki kipute hicho imepangwa kufanywa kesho Jumatano tarehe 21 Agosti ugani Umeme Ziwani, Nairobi. Kocha wa Pumwani Sports, David Onyango anashikilia kuwa vijana wake wamejiandaa kiume kutetea taji hilo.
''Tayari taji la ligi ya NairobI Mashariki limeenda ambapo sasa tuna geukia kupigania ubingwa wa Kothbiro Cup,'' anasema kocha wa Pumwani Sports, David Onyango.
Jumla ya timu 32 zimethibitisha kushiriki ngarambe ya mwaka huu. Shindano hilo hujumuisha timu kutoka maeneo tofauti nchini ikiwamo Nairobi, Kiambu na Kajiado kati ya mengine.


