top of page
Search

KVF Yazindua Tovuti , Mipango ya Kutangaza Mchezo Huo Kimataifa

  • heartmediak4
  • Oct 30, 2024
  • 2 min read

Na HEART MEDIA

Jumatano 30, Oktoba 2024.



SHIRIKISHO la voliboli ya Kenya (KVF) limezindua tovuti itakayokuwa ikipakiwa habari zote kuhusu mchezo huo nchini.Tovuti hiyo itapakiwa habari kuhusu makocha wa voliboli pia habari za mastaa tofauti wanaume na wanawake nchini. Pia habari za Ligi kuu na mashindano tofauti pia matokeo ya mechi tofauti za mchezo huo nchini bila kuweka katika kaburi la sahau histori ya timu za taifa kaika mashindano ya kimataifa. Kadhalika ilitangaza kuwa mechi za Ligi Kuu msimu mpya zitakunjua jamvi mapema Alhamisi hii tarehe 31 Oktoba 2024.




Hafla ya uzinduzi huo iliandaliwa katika kituo Cha KCB Leadership Centre, Karen Nairobi Jumanne tarehe 29 Oktoba 2023. Akitangaza hayo rais wa KVF, Charles Nyaberi alisema kuwa wamepania kuanzisha shindano la Kenya Cup mapema mwaka ujao litakaloshirikisha timu za Wanaume na wanawake. Rais huyo alisema kuwa watakuwa wazipatia nafasi timu tatu za kwanza katika jedwali ya ligi kuu, wanaume na wanawake kushiriki shindano la Klabu Bingwa AFfrika (CAVB). Kisha nafasi ya nne na tano zitakuwa zinapewa nafasi kushiriki shindano la Ukanda wa Tano (Zone five).


"Tumepania kupaisha mchezo wa voliboli nchini Kwa timu za taifa wafalme stars na malkia strikers," alisema. Alishukuru wafadhali wote ambao wamekuwa wakiwashika mkono ikiwamo Mozzartbet, Java House, Kenya Pipeline na KCB kati ya wengine.



Kadhalika alitoa wito Kwa wadhamini zaidi kujiunga na KVF kwenye juhudi za kukuza atalanta za wachezaji chipukiz wa mchezo huo.


"Uzinduzi wa mipango ya KVF ni muhimu zaidi kwenye juhudi za kukuza voliboli nchini," alisema ofisa Wa KCB, Judith Sidi Odhiambo. Ofisa huyo aliunga mkono mpango wa KVF wa kukuza Atalanta za wachezaji chipukizi sambamba na benki hiyo.


Naye ofisa wa mauo wa Mozzartbet, Frank Ochieng alishukuru ushirikiano wa shirika hilo na KVF kwenye juhudi za kuhakikisha timu za mchezo huo zinazidi kubeberusha bendera ya Kenya kimataifa. '' Tunafahamu kandarasi yetu na KVF ya kupiga jeki Malkia Strikers itakatika mwishoni mwa mwaka huu lakini tunawazia suala la kuirefusha,'' alisema. Aliongeza huwa wana kibarua kigumu wakati wanapofadhili mchezo wowote maana ni muhimu kutoa ufadhili kisha kupata matunda mema.


Naibu kocha David Kirwa Wa GSU alipongeza KVF Kwa kuanzisha tovuti na kusema itasaidia kutangaza wasifu wao kimataifa. Kuhusu mechi za ligi kuu msimu huu alisema wamejiandaa vya kutosha tayari kuanza kampeni zao kupigania taji hilo ambalo wamelikosa ndani ya misimu miwili baada ya kushinda mara tanoi mfululizo.


 
 
bottom of page