Kariobangi Legends Wazee na Black Stars Wazee Kukipiga Jumapili Ijao
- heartmediak4
- Nov 19, 2024
- 1 min read
Na HEART MEDIA
Jumanne 19, Novemba 2024

TIMU ya Kariobangi Legends Wazee imepania kupiga patashika tatu ugenini japo za kupimana nguvu. Mwenyekiti wa klabu hiyo, Eric Otieno Atanga amefunguka hayo na kuserma kuwa wanalenga kushiriki mechi hizo kwenye viwanja tofauti kando na ardhi ya nyumbani.
''Tumecheza mechi nyingi katika uwanja wa nyumbani ambapo ni muhimu tujaribu kubadilisha hewa ili kujipima kama tutaendeleza rekodi ya kushinda mechi zetu,'' anasema bosi huyo. Anatoa wito kwa wachezaji wake kujitolea na kusafiri kushiriki mechi za ugenini. Alidokeza hayo juzi Jumapili tarehe 17 Novemba 2024, muda mfupi baada ya mechi yao dhidi ya Mwiki Legends kuhairishwa.

Kariobangi Legends Wazee sasa inajiandaa kushiriki mechi ya kurafiki Jumapili ijayo tarehe 24, Novemba 2024 dhidi ya Black Stars Wazee uwanjani Jamhuri Park, Nairobi.
Kocha wa Kariobangi Legends Wazee, Kelvin 'Odengo' Otieno anasema ana imani kama kawaida wachezaji wake watafanya kweli kwenye mchuano huo.
Kariobangi Legends Wazee imeibuka moto wa kuotea mbali kwenye michuano ya kirafiki. Kwenye mechi iliyocheza wiki iliyopita, Kariobangi ilibeba ufanisi wa mabao 2-1 mbele ya Dandora Legends. Kwenye matokeo chache ya wiki zilizotangulia kikosi hicho kilikandamiza Githurai 45 Wazee kwa magoli 5-1 kisha kuagana mabao 3-3 dhidi ya Baba Dogo Legends


