top of page
Search

Kariobangi Legends Wazee Mtaikoma Mazee

  • heartmediak4
  • Oct 25, 2024
  • 1 min read

Na HEART MEDIA

Ijumaa, 25 Oktoba 2024




BILA shaka Kariobangi Legends Wazee inazidi kukomaa kinoma kwenye migarazano ya kirafiki dhidi ya wapinzani wao katika Kaunti ya Nairobi. Kariobangi Legends Wazee imebeba ushindi wa patashika moja sawa na kutoka nguvu sawa mara moja kwenye mechi ilizocheza ndani ya siku tatu zilizopita. Ikiongozwa na kocha, Philip Munyoki ilikandamiza Githurai 45 Wazee kwa magoli 5-1 kisha kuagana mabao 3-3 dhidi ya Baba Dogo Legends.



Kwenye mechi ya kwanza kikosi hicho kilitembeza soka safi na kuashiria kama kawaida imepania kuendeleza rekodi ya kutoshindwa. Timu hiyo iling'aa mbele ya wapinzani wao huku ikionyesha ushirikiano mwema dimbani kupitia wachezaji kama Geoffrey Wangalwa, Hillary Otieno na Philip Munyoki kati ya wengine. ''Bila kusifia wachezaji wangu huwa sio rahisi kushindwa kwenye mechi zetu kwani kila wakati hulenga kufanya kweli,'' anasema meneja wa kikosi hicho, Julius Agwaya. Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji waliowahi kusakatia timu tofauti katika ujanja wao. Kariobangi Legends Wazee inajivunia kumaliza ya pili kwenye ligi ya wazee pamoja Kaunti ya Nairobi msimu uliyopita. Nayo ABSA Legends ilijitahidi kiume na kuhifadhi ubingwa huo iliyokuwa imetwaa muhula uliyotangulia.

Kwenye mechi za hivi karibuni Kariobangi Legends Wazee ilipiga 44 Legends kwa mabao 2-0, ilibeba magoli 5-1 mbele ya Mathare North Legends.



 
 
bottom of page