top of page
Search

Kariobangi L. Youth, Gikuni Utd Kazi Imeanza Daraja la Pili

  • heartmediak4
  • Nov 5, 2024
  • 1 min read

Na HEART MEDIA

Jumanne, 5 Novemba 2024




KARIOBANGI Legends Youth ilikandamiza Utafiti FC kwa mabao 5-0 kwenye mechi ya Kundi C kuwania taji la Ligi ya Taifa Daraja la Pili iliyopigiwa uwanja wa Kari Kikuyu. Kwenye mechi hizo zilizochezwa Jumamosi na Jumapili tarehe 2, Novemba na tarehe 3, Novemba 2024, Gikuni United ilisajili ufanisi wa mabao 3-1 mbele ya Thika Sporting.

Kariobangi iliyoanza kampeni zake kwa kuzamisha Gikuni United iliteremsha sofa safi ikilenga kuhakikisha imefanya kweli na kujiongezea alama mbili muhimu. Ushirikiano mwema dimbani ulichangia matokeo ya kuridhisha. Kariobangi Legends Youth ilipiga wapinzani hao kupitia juhudi zake Bramwel Kavaya, Brian Idalia, Ben Muna, Idris Amadi na Abdallah Siraji. ''Tunapongeza wachezaji wetu kwa kuonyesha ushirikiano mwema na kuhakikisha wametia kapuni pointi tatu muhimu hali inayoweka wazi kuwa wanalenga kufanya kweli,'' anasema mwenyekiti wa Kariobangi, Eric Oteino Atanga.

Anaongeza kuwa endapo kikosi hicho kitaendeleza mtindo huo kitafanya kazi ya kupendeza na kuzoa tiketi ya kupandishwa ngazi. Anashikilia kuwa hawapo tayari kushiriki kipute hicho mara mbili bali wamepania kuhakikisha wanashiriki kila ligi kwa msimu mmoja na kupanda ngazi.



Nayo GikuKariobangi ni ilifanya kazi ya kupendeza na kuhakikisha imetia kapuni ufanisi wa pointi tatu muhimu. Vijana hao walinyanyua ushindi kupitia makombora ya Ezra Mutai, Geoffrey Kariuki na Abdiaziz Hassan.

Kwenye mfululizo wa matokeo hayo, Royal Fresh FC ilizamisha Tusker Youth kwa mabao 3-1, nao vijana wa City Sports waliadhibu Kikuyu Township kwa magoli 3-0 huku Githurai All Stars (GAS) ikituzwa ushindi wa mezani baada ya Nyahururu Griffon kuingia mitini na kukosa kufika jkushiriki mchezo huo. Nao wachana nyavu wa Blue Nile FC waliangushwa kwa mabao 3-1 na South C Rangers FC.



 
 
bottom of page