top of page
Search

Handiboli: Mashindano ya Super Cup Kuandaliwa Mapema mwezi Ujao

  • heartmediak4
  • Jul 18, 2024
  • 2 min read

Na HEART MEDIA

Alhamisi, 18 JULAI 2024


NGARAMBE ya handiboli kuwania taji la Super Cup ambayo huandaliwa kabla ya mechi za msimu mpya kukunjua jamvi sasa imepangwa kuandaliwa mapema mwezi ujao (Agosti 2 hadi 4). Shindano hilo hushirikisha timu zilizoibuka nafasi sita bora na nne bora katika jedwali la ligi kuu ya wanaume na wanawake mtawalia. Maafande wa Jeshi la Ulinzi (KDF) na vipusa wa Nairobi Water Queens ndio mabingwa watetezi kwenye kipute cha mwaka huu.


Ushindani mkali unatazamiwa kushushwa kama ilivyokuwa kwenye kampeni za ligi kuu msimu uliyokamilika mwezi Mei mwaka huu. Kwa mara ya kwanza ndani ya misimu 11 upinzani mkali ulichangia warembo wa Nairobi Water Queens kupoteza ubingwa huo. Vipusa hao wa kocha, Jack Ochieng walikuwa wamebeba taji hilo kwa kipindi hicho ambapo kwa jumla walikuwa wamepoteza mechi moja pekee katika ligi zote. Kwenye michuano ya msimu uliyopita taji hilo lilitwaliwa na Maafande wa Jeshi la Ulinzi (KDF).


''Bila shaka tuna imani wakali wa mchezo huo nchini watateremsha ushindani wa kufa mtu kama tulivyoshuhudia kwenye michuano ya ligi,'' alisema katibu mpango ratiba wa mchezo huo, Charles Omondi. Aliongeza kuwa ana furaha maana mchezo huo unaonyesha dalili za kuimarika licha ya kuwa imekuwa vigumu kupata wafadhili kuwapiga jeki. Meneja wa Nairobi Water Queens, Caroline Kusa anadokez kuwa lazima wahifadhi taji hilo hasa baada ya kupokonywa taji la Ligi Kuu muhula uliyopita. ''Katika mpango mzima tumejiandaa vilivyo kunyamazisha wapinzani wetu kusudi tujifariji kwa kutwa ubingwa wa Super Cup,'' alisema.

Kitengo cha wanaume timu zishiriki zimegawanywa kwa makundi mawili.

Kundi A linashirikisha: Halmashauri ya Nafaka na Mazao nchini (NCPB), Equity Bank, Starthmore University huku Kundi B likijumuisha: KDF, Kenya General Service Unit (GSU) na Black Mamba. Kitengo cha wanawake kampeni hizo zitashirikisha KDF, Nairobi Water Queens, NCPB na Rangers.



 
 
bottom of page