top of page
Search

Black Stars Wazee Yaona Moshi Dhidi ya Kariobangi Legends Wazee Japo Kirafiki

  • heartmediak4
  • Nov 25, 2024
  • 1 min read

Na HEART MEDIA

Jumatatu 25, Novemba 2024






TIMU ya Black Stars Wazee imeshindwa kutamba mbele ya Kariobangi Legends Wazee kwenye mchuano wa kirafiki uliochezewa uwanja wa Jamhuri Sports Complex, Nairobi. Kwenye mechi hiyo iliyochezwa Jumapili tarehe 24, Novemba Kariobangi Legends Wazee iliendeleza rekodi ya kufana ilipoadhibu wenyeji wao kwa mabao 4-1.




Patashika hiyo ilichezwa wiki moja baada ya mwenyekiti wa kikosi hicho, Eric Otieno Atanga kutaja kuwa wanalenga kushiriki takribani mechi tano ugenini ili kupima wachezaji wao. Wachezaji wa Kariobangi Legends Wazee waliendelea kushusha soka safi kwenye mfululizo wa mechi zake. Kikosi hicho kilishuka dimbani kwa kasi lengo nikiwa moja kuhakikisha kinashinda mchuano huo.


Wanasoka hao walifunza wenzao soka na kuhakikisha wanabeba ushindi mtamu. Katika patashika hiyo, Sammy Muring'u na Evans Kaule kila mmoja alitikisa wavu mara mbili na kuhakikisha kikosi hicho kinazidi kufanya kweli. Kocha wa Kariobangi Legends Wazee, Kelvin 'Odengo' Otieno anasema wachezaji wenzake walifanya kazi nzuri lakini sio jinsi walivyotarajia. ''Kiukweli tulipania kuvuna ushindi mkubwa kwa idadi ya magoli lakini ni vizuri hatukushindwa,'' anasema. Anaongeza kwamba kama kawaida wamepania kuendelea kunyamazisha wapinzani weo kwenye mechi zijazo.



Kariobangi Legends Wazee imeibuka moto wa kuotea mbali kwenye michuano ya kupimana. . Kwenye mechi iliyocheza wiki kadhaa zilizopita, Kariobangi ilibeba ufanisi wa mabao 2-1 mbele ya Dandora Legends. Kwenye matokeo mengine kikosi hicho kilikandamiza Githurai 45 Wazee kwa magoli 5-1 kisha kuagana mabao 3-3 dhidi ya Baba Dogo Legends.

 
 
bottom of page