Assassins, Sparrows Za KU Mtazikubali Voliboli ya NANOKUSF
- heartmediak4
- Oct 8, 2024
- 2 min read
Na HEART MEDIA
Jumanne, 8 Oktoba 2024

TIMU za Chuo Kikuu cha Kenyatta (KU) maarufu Assassins na Sparrows kitengo cha wanaume na wanawake mtawalia zimepania kukiwasha kwenye voliboli ya Vyuo Vikuu vya Kenya Kanda ya Nairobi Kazkasini (NANOKUSF). Kocha wake, Vitalis Ojukwu anasema kuwa hawana la ziada bali wanalenga kuendeleza ubabe wao kwenye michuano hiyo huku wakijinolea fainali za Afrika Mashariki na Kati (FEAUS) zitakaoandaliwa hapa nchini mwezi Desemba mwaka huu. Vikosi hizo zimetoa dalili za kutesa baada ya kila moja kusajili ushindi wa tatu kwenye mechi za raundi ya tatu zilizochezwa Jumapili tarehe 6, Oktoba 2024. .

Kwenye matokeo hayo, wanaume wa KU waliangusha USIU-A kwa seti 3-0 (25-17, 25-15, 25-21) nao warembo walisajili seti 3-0 (25-11, 25-13, 25-19) mbele ya USIU.
''Jambo tunalofahamu ni kuwa timu zote ni waasidi wakuu wala hakuna ya kupuuza,'' anasema kocha huyo. Anaongeza kuwa wamepania kukaza buti zaidi kusudi kujiweka vizuri kwa ajili ya michuano ya FEAUS.
Kwenye mfululizo wa matokeo hayo kwa wanaume, Jomo Kenyatta (JKUAT) ilibeba ushindi wa seti 3-1 na 3-0 mbele ya St Pauls University (SPU) na Taasisi ya Mama Ngina (MNUC) mtawalia. Nayo Mount Kenya University (MKU) ilinyuka Gretsa seti 3-0 huku KCA ilikilala kwa seti 3-2 mbele ya Daystar.
Kitengo cha wanawake, Gretsa ilicharaza MNUC seti 3-0, nayo KWUST ilisajili seti 3-0 na 3-1 mbele ya Gretsa na KCA mtawalia, MKU iliadhibu JKUAT seti 3-1 na kubamiza Daystar seti 3-1, USIU ilifinywa kwa seti 3-0 na JKUAT huku KCA ikipepeta MNUC kwa seti 3-0.
MAGONGO
Kwenye mpira wa magongo ya wanaume, Jomo Kenyatta (JKUAT) ilipiga KCA 2-0, St Pauls University (SPU) ilizaba Parklands 2-1, KU ilitoka nguvu sawa mabao 2-2 dhidi ya Daystar University, SPU iliagana bao 1-1 na JKUAT nayo MKU ilizaba Daystar kwa mabao 3-0. Kitengo cha wanawake:KU ilibeba ushindi wa mechi mbili kwa mabao 3-0 na bao 1-0 dhidi ya Daystar na JKUAT mtawalia. Hata hivyo JKUAT ilizamisha SPU kwa mabao 11-0 nayo MKU ilitoshana nguvu bao 1-1 na USIU.

SOKA
Katika soka ya wanaume, KU ilifyeka Gretsa kwa mabao 9-1, JKUAT iliumwa na KU Parklands mabao 2-1, KCA ilitandika MKU Nairobi mabao 5-0, USIU ilidunga MNUC kwa bao 1-0, SPU 1-1 Daystar, Daystar 2-2 PAUSTI. Kwa kina dada: JKUAT 2-0 Gretsa, SPU 2-0 USIU, KU 2-0 KU Parklands, KCA 3-2 Daystar, KWUST 6-0 MNUC.
HANDIBOLI
Kwenye handiboli ya wanaume:KU 60-18 KCA, Daystar 58-20 MNUC, JKUAT 15-00 Gretsa, SPU 30-27 MKU nao vipusa wa MNUC 04-13 Gretsa. Kwenye mpira wa pete kitengo cha wanawake:MNUC 18-32 SPU, MKU 53-30 USIU, Gretsa 00-60 KU, KWUST 41-29 JKUAT nayo Daystar 58-04 Daystar City.
MPIRA WA KIKAPU
Kwenye mechi za kikapu ya wanaume: MKU 55-35 SPU, JKUAT CBD 55-46 MKU, USIU 20-00 MNUC, Daystar 52-63 Gretsa. Kwenye matokeo ya wanawake: SPU 11-32 KCA, JKUAT 102-14 Daystar, USIU 113-10 KWUST na KU 33-41 MKU.


